NDANI YA BONGO: Vodacom Stars

Hizi ndizo habari njema sasa ndani ya bongo, mji wa wajuzi wa kubonga, kuhonga, na kukomba visivyo vyao. Baada ya siku ndefu ya kutumikia mafisadi, unarudi nyumabi na uchovu wa msukule wa siku nzima wa kuwatumikia mabwana mafisadi. Baada ya siku ndefu unarudi nyumbani kusikokuwa na umeme, maji, bali kelele za mbu na mama watoto, umasikini kitu kingine acheni. Lakini unapoketi na kunyakua gazeti na kukutana na habari hii, ninauhakika lazima itakutabamusisha japo kidogo. Nimefurahi kujua bongo kuna program kama hii ya kukuza vipaji kwa vijana, hasa kwenye soka, mchezo nambali moja Tanzania. Simba na Yanga wameishia wapi hii leo na utani wa jadi. Huo utani ulikuwa enzi zile bwana, kila masikio redioni mkipandishwa hamasa na midadi ya mtangazaji mpira wa radio Tanzania, aahh enzi zile bwana. Siku hizi Yanga na Simba wanasua sua tu, kwani akiba ya vipaji bongo imepungua. Program kama hizi Simba na Yanga miaka nenda rudi wamekuwa wakiambiwa waanzishe, wakuze vipaji vyao, kwani hamuoni Ulaya wanavyofanya. Sasa naona Vodacom wanafanya kweli kwenye mpira, safi sana. Hongera nyingi kwa Vodacom kwa kuwekeza kwa vijana wakati wazee wa kutengeneza sera wakiishia kupiga domo tu….sasa wabongo igeni yaliyo na manufaa basi sio kama hayo ya Ali Kiba na tshirt zao za FREE T.I.D, how pathetic, nimemaliza.